IGP Sirro Afunguka Kuhusu Mwandishi Aliyepigwa na Polisi

IGP SirroAfunguka Kuhusu Mwandishi Aliyepigwa na Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP ,Simon Sirro ametoa ufafanuzi juu ya Sakata la Mwandishi wa Habari aliyepigwa na polisi wakati akitekeleza majukumu yake katika Uwanja wa Taifa ulioko jijini Dar es Slaam na kusema kuwa upelelezi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli wa tukio hilo na kuchukua hatua stahiki za kisheria na  kulinda heshima ya jeshi la polisi.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akiwasili jijini Arusha kwa ziara yake ya kutembelea eneo la Mto wa Mbu ambapo yalitokea matukio ya wanawake kubakwa na kuuawa ,ziara ambayo inalenga kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa matatizo hayo ikiwa ni kuimarisha ulinzi na kuongeza idadi ya pilisi.



Sirro amesema kuwa vyombo ya usalama vinaendelea na upelelezi kujua ukiukwaji huo wa sheria iwapo ni polisi pekee ama mwandishi huyo alikiuka sheria na maagizo ya polisi ili waweze kujiridhisha na kuchukua hatua.

Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi amezungumzia uchaguzi mdogo uliofanyika na dosari chache zilizosababisha na baadhi ya watu kufanya vurugu na kuwataka polisi kukamilisha upelelezi ili wafikishe mahakamani na kuchukuliwa hatua ,ikiwa ni pamoja na ziara yake katika eneo la mto wa Mbu.

Kwa Upande wake Mkazi wa Jiji la Arusha Gephrey Stephen amesema kuwa licha ya serikali kutambua mchango wa Wanahabari bado kuna changamoto kwa jeshi la polisi linapaswa kujitathmini mahusiano yake na wanahabari pamoja na wananchi kwa ujumla.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad