Wazazi/Walezi wa Mtoto huyo wameongea na millardayo.com na AyoTV Kagera na kueleza kuwa Mtoto huyo hakuwa mwizi, alijitahidi kusoma kwa bidii ili baadae aje kutimiza ndoto yake ya kuwa Mwanasoka bora duniani.
Mtoto huyu alifika kwenye mikono ya Mlezi baada ya kufiwa na Mama yake baada ya kuzaliwa, Mlezi wake ambae ni Mchungaji aitwae Justus ndie aliemlea toka akiwa na mwaka mmoja ambapo alimchukua kutoka kwenye kituo cha kulea Watoto Yatima.
Mpaka sasa ambapo alikua darasa la tano hakuwa amejua Baba yake ni nani kwasababu alikua akilelewa kama Watoto wengine nyumbani, maelezo kamili yapo kwenye hii video hapa chini.