Instagram kwa sasa wamefanya maboresho matatu makubwa kati ya maboresho matano ambayo kampuni hiyo iliahidi mwanzoni mwa mwaka huu kuwa itayaleta ndani ya mwaka huu, na tayari kampuni hiyo imeanza kuyafanyia kazi.
1-KUOMBA MAOMBI YA UTAMBUZI WA AKAUNTI YAKO MOJA KWA MOJA (Request Verification) ILI KUPATA ALAMA YA TIKI.
Mwanzoni mitandao karibia yote mikubwa ya kijamii isipokuwa Instagram ilikuwa na options ya mtumiaji kujaza fomu ya kuomba utambuzi wa akaunti yake ili aweze kupata tick ya blue. Hii ililetwa ili watumiaji waweze kutofautisha kati ya akaunti fake na halali pia iwe rahisi kutofautisha akaunti hizo.
Habari nzuri ni kwamba nao Instagram wameanza kuruhusu huduma hiyo ambapo watu maarufu wakiwemo wasanii, wanasiasa, wanamichezo, wanamitindo na hata makampuni yataomba kupata verification badge.
Sehemu hiyo inapatikana mwisho kabisa kwenye Setting ya App ya Instagram ambapo utaona neno Request Verification na utabofya na kisha kujaza fomu.
2-MABORESHO MAKUBWA YA ULINZI WA AKAUNTI YAKO ILI KUJIKINGA NA WADUKUZI.
Mwanzoni Instagram ilikuwa na njia moja tu kubwa ya ulinzi ambayo watumiaji wake walikuwa wanatumiwa code kupitia namba husika ya simu ili waweze ku-log In. Ishu ambayo ilikuwa bado inaleta changamoto kwa watumiaji wake kwani bado wadukuzi walikuwa wanaendelea kudukua.
Sasa maboresho ya sasa kuhusu udukuzi suala hilo litabaki kuwa ni historia kwani Instagram wameleta njia nyingine mbili za kuilinda akaunti yako. Njia hizo ni kwa kutumia App nyingine kwa ajili ya usalama wa akaunti yako na App hizo ni Authy 2-Factor Authentication na Google Authenticator ambazo App zote mbili zitahusika kulinda akaunti yako dhidi ya wadukuzi.
Pia ili kupata ulinzi huo ingia Settings na kisha bonyeza Two Factor Authentication na utaona sehemu hizo mbili za ulinzi zitakazokupa maelekezo zaidi.
Maboresho yote haya yameanza kufanya kazi karibia duniani kote ambako App ya Instagram inafanya kazi ili uweze kufaidi, Update kwanza hiyo Programu yako kwenye simu za Android na iOS.
Bongo5