Iran Yagomea Mazungumzo ya Nyuklia na Marekani

Iran Yagomea Mazungumzo ya Nyuklia na Marekani
Iran imesema haitaingia kwenye raundi mpya ya mazungumzo ya nyuklia na Marekani kutokana na Marekani kutumia "Ubabe na Ulaghai" kwenye mazungumzo.

Akiongea kuhusu nia ya Marekani kutaka kuwa na mazungumzo na Iran bila masharti, Kiongozi mkuu wa Iran Ayatollah Ali Kamenei amesema Iran haitakaa tena kwenye meza ya mazungumzo na serikali ya "kilaghai" ya Marekani.

Ayatollah Khamenei amesema wakati wa majadiliano wamarekani wanatoa maneno ya uhakikisho, lakini wao wanataka upande mwingine uwaitikie kivitendo na wao hawakubali ahadi.

Amesema majadiliano na Marekani kwa sasa hayatakuwa na manufaa kwa Iran, na yanapigwa marufuku.

Mapema kabla ya hapo waziri wa mambo ya nje wa Iran Bw.Javad Zarif alikanusha habari kuwa Marekani ina nia kufanya mazungumzo ya pembeni na Marekani kwenye mkutano ujao wa Umoja wa mataifa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad