Irene Uwoya "Bado Sijaona Kama Kanumba"

Mwigizaji mama la mama kwenye kiwanda cha kuzalisha Bongo Movies, Irene Pancras Uwoya ametoa la moyoni kwamba, bado hajaona mtu kama marehemu Steven Kanumba kwenye tasnia hiyo.

 Uwoya ambaye ni mama wa mtoto mmoja wa kiume, Krish Ndikumana aliiambia Over Ze weekend kuwa, Kanumba ni staa aliyekuwa anajitoa ili kuifikisha Bongo Movies mbali, jambo ambalo hakuna anayelifanya kwa sasa.

 “Wakati mwingine alikuwa anatoa pesa yake mwenyewe mfukoni ili tu kufanya jambo la kuipeleka Bongo Movies mbali na kweli alikuwa ameanza kufanikiwa kuitangaza Tanzania duniani,” alisema Uwoya ambaye amecheza filamu nyingi na Kanumba.

NEEMA ADRIAN

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad