Italia Yautaka Umoja wa Ulaya Kuheshimu Makubaliano Yao Juu ya Wahamiaji

Italia yautaka Umoja wa Ulaya kuheshimu makubaliano yao juu ya wahamiaji
Naibu waziri mkuu nchini Italia Luigi di Maio, ametishia kuacha kuchangia fedha katika Umoja wa Ulaya mwaka ujao, vinginevyo wanachama wa umoja huo wawachukue wahamiaji karibu mia moja na hamsini waliomo katika meli nchini Sicily.

Katika ukurasa wake wa Facebook,naibu waziri mkuu Di Maio, amesema ikiwa mkutano wa kamisheni ya Umoja wa Ulaya unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii utashindwa kupata suluhisho,harakati za nchi zenye hadhi ya nyota tano hazitakuwa tayari kutuma euro bilioni ishirini nchini Brussels.

Kwa nini Wakenya wameorodheshwa kuwa wahamiaji wenye bidii zaidi nchini Marekani?
Vijana ishirini na saba waliruhusiwa kuondoka katika meli inayoshikiliwa , ingawa waliosalia wako katika pwani ya Italia ambapo meli ya ulinzi mali ya Italia iliwaokoa kutoka bahari wiki iliyopita.

Waziri wa mambo ya ndani nchini humo Matteo Salvini amezishutumu nchi za Umoja wa Ulaya kwa kuvunja ahadi zao za kuchukua wahamiaji kutoka meli ya awali ya uokoazi ambayo iliruhusiwa kwenda Italia.

Na kuongeza kusema kuwa wahamiaji hao walitaka kutelekezwa na Italia haina ruhusa kuokoa wahamiaji baharini kwa muujibu wa sera na sheria zake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad