January Makamba Atoa Ushauri Kwa Viongozi Vijana Walioteuliwa


Ni siku kadhaa zimepita tokea Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dr John Pombe Magufuli ateue viongozi mbalimbali katika ngazi ya Wilaya na Mikoa na tuliona watu mbalimbali wakitumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kutoa pongezi kwa viongozi hao.

Kupitia mtandao wa twitter katika page ya Waziri wa Nchi ofisi ya makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makambaameonekana kutoa ushauri kwa viongozi vijana walioteuliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.

January Makamba ameandika “Mdogo wangu uliyepata nafasi ya uongozi, jitahidi kukataa, kufunguliwa mlango wa gari, kubebewa mfuko au sahani ya chakula kwenye buffet, kulazimisha kukaa meza kuu au kutambuliwa kwenye shughuli za watu. Wenyeji wanaweza ku-insist lakini resist, waweza kushindwa lakini jitahidi”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad