Je Mafuta ya Nazi ni Sumu Kali? Soma Hapa Inakuhusu

Iwapo umekuwa ukidurusu mitandao wiki hii , ni wazi kwamba umepata kuona kwamba mafuta ya nazi ni 'sumu halisi' na sio tiba kama ilivyodhaniwa. Inaonekana kama kutia chumvi-lakini sio chumvi mbaya hata hivyo.

Lakini onyo hilo lililozua maswali mengi linatoka kwa Karin Michels , profesa wa tawi linalohusiana na magonjwa katika chuo kikuu cha Havard aliyetoa hotuba yake mjini Freiburg Ujerumani ambayo baadaye iliwekwa katika mtandaoi wa You Tube.

Kama anavyosema profesa Michels , katika hotuba hiyo ambayo imetazamwa zaidi ya mara milioni moja , mafuta ya nazi ni miongoni mwa vyakula vibaya zaidi kula.

Chakula kilicho na mafuta mengi kinaweza kusababisha madhara katika viungo vyako vya ndani.Sisi sio wageni wa kuambiwa kwamba chakula tunachokula kina madhara mwilini mwetu.

Kumbuka tulipoambiwa kwamba nyama ya nguruwe inasababisha saratani, ama kwamba mvinyo mwekundu sio mzuri kwa afya yetu.

Na wiki iliopita pekee tulipogundua kwamba , licha ya miaka kadhaa ya kuambiwa visivyo kwamba vyakula visivyo na madini ya kabohydrayte vinaweza kupunguza miaka ya maisha yako.

Ni wazi kwamba Profesa Michels sio mtu wa kwanza kusema kwamba mafuta ya nazi yana mafuta mengi na ni mabaya .

Mwaka 2005 - miaka 13 iliopita -shirika la afya duniani lilikuwa limeorodhesha mafuta ya nazi kuwa ,miongoni mwa vyakula ambavyo havifai kutumiwa kama chakula kama hutaki kupatwa na mshutuko wa moyo.

Miaka ya 90 kulikuwa na tahadhari ya kiafya nchini Marekani wakati utafiti ulipodai kwamba 'popcorn' zinazotumika wakati watu wanapotazama filamu zina mafuta kwa sababu zilikuwa zikipikwa katika mafuta ya nazi.

Wakati huohuo hatahivyo mafuta ya nazi yamekuzwa kama chakula kizuri cha kiafya.

Kulingana na utafiti kutoka kwa muungano wa American Heart mwaka uliopita , takriban asilimia 72 ya raia wa Marekani wanaamini kwamba mafuta ya nazi yana afya-hata ijapokuwa katika kiwango hicho ni asilimia 37 ya wataalam wa lishe bora wanaokubali.

Tofauti iliopo , wanasema inatokana na kampeni nzuri za ukuzaji kutoka kwa makampuni ya kuuza mafuta hayo ambazo zinasema kuwa yanaweza kutumika kama mbadala wa siagi na mafuta ya yanayotokana na mimea mbali na ithibati kutoka kwa watu maarufu kama Gwyneth ambaye amepiga debe kutumia kama chakula bali pia kutumia kama mafuta ya kupaka uso na nyewele.

Utumizi wa mafuta ya nazi kujipaka mwilini mbali na kutia nyweleni ni mambo ya kawaida nchini India swala ambalo huenda limechangia mafuta hayo kupendwa sana kiafya.

Mbabe wa zamani wa kivita DRC azuiwa kuwania urais
Victoria taylor afisa mwandamizi kuhusu lishe bora katika wakfu wa British Heart , aliambia BBC Three kwamba Profesa Michel yuko sawa licha ya kampeni kubwa ya kukuza mafuta hayo.

Mafuta ya nazi yamejaa mafuta asilimia 86-ambayo ni thuluthi moja zaidi ya siagi , kulingana na victoria.

Wengine wamesema kuwa mafuta ya nazi yametumika kama kiungo katika tamaduni nyengine hususan Afrika, Asia na kusini wa marekani kwa karne kadhaa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Labda waseme hiyo teknologia ya sasa ya kilimo inayolenga kuangamiza organic food, pengine ndo mbaya. Nasikitika nchi za Africa, ikiwemo tz imeamua kuchangamkia mageuzi hayo ya kilimo eti ili kuondoa ufukara kwa wskulima. Wito wangu kamwe tz tusikubali kucomply. Waziri wa kilimo, ipe hiyo idea km pilot programme tu. Matajiri wanaopromote hicho kilimo cha GM wenyewe, pengine wanakula organic food, sababu wanauwezo wa kuaford organic food ambayo ni ghali kwa bei. Walala hoi ndo wateja wa gmo. Tafiti zinasema Walala hoi hufa wakiwa vijana kuliko Matajiri, pia Walala hoi ndo huumwa mgonjwa ya kisukari moyo saratani kadhaa homa za mapafu nk

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad