Kuna Shangazi yangu anaolewaa , ni Single mother, tayari ana mtoto mmoja wa miaka 5.
Kama mjuavyo, kitchen party na send off huwa ziko chini ya upande wa mwanamke. Hivyo jukumu tunalibeba sisi wana ndugu.
Huyu Shangazi yangu, kiuchumi yupo vizuri, ana kiduka chake k.koo hivyo ana jimudu.
Sasa kapata mchumba wa kumuoa, na taarifa zishafika kwa wazee. Taratibu zote zimefuatwa kilicho baki ni kuolewa.
Sasa mkasa mzima ni yeye kutaka kufanyiwa Kitchen Party, na Send-off. Na kama mjuavyo kinachofuata hapo ni michango.
Wanandugu wamegawanyika, wengine wakidai Sherehe kama hizo ni kwa Mwanamke ambae hakuwahi kujifungua, au kuishi nawanaume.
Mwanamke anae fanyiwa kitchen party na send off ni kama pongezi kwa kuweza kujitunza mpaka kufikia hatua ya kuolewa kwa heshima bila kuzaa nje ya ndoa.
Lakini wazazi wake wana komaa, wanadai wao wamechangia shughuli za watu wengi sana, hivyo mwanao anapaswa kutendewa haki kama wengine.
Wakuu, kwa nyie mnaonaje hili?