Jean Pierre Bemba Kurejea Nchini Congo

Jean Pierre Bemba Kurejea Nchini Congo
Kiongozi wa upinzani nchini Kongo, Jean Pierre Bemba anatarajiwa kurudi nyumbani siku ya leo, baada ya kukaa kwa takribani muongo mmoja akiwa kifungoni na nje ya nchi ya Kongo.

Bemba alifutiwa mashataka hivi karibuni na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ICC, aidha ameonesha wazi nia yake ya kugombea Urais nchini Demokrasia ya Kongo. Alishindwa katika uchaguzi wa mwaka 2006 dhidi ya Rais wa sasa Joseph Kabila ambaye muda wake umeisha tangu mwaka 2016, jambo ambalo bado linaleta maswali mengi kama ataogombea tena.

Kurejea kwa Bemba DRC kutakuwa na maana gani?

Biashara ya Benki Tanzania yasuasua kutokana na wateja kutolipa madeni

Kurudi kwa Bemba kunatarajiwa kusisimua upya na kutikisa siasa za Demokrasia ya Kongo, chama tawala tayari wametoa tamko kuwa Bemba hana vigezo vya kugombea nafasi ya urais nchini humo, kutokana na alikua mshitakiwa wa mahakama ya makosa ya jinai ICC.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad