Kufuatia Tukio la kushambuliwa kwa kupigwa kwa mwandishi wa habari lililozidi kushika kasi na kukemewa na viongozi na taasisi mbalimbali nalo jeshi la polisi ambalo ni mtuhumiwa wa kwanza kutokana na kuonekana baadhi ya askari wake wampiga mwandishi huyo kupitia kamanda wa polisi wa kanda maalum Lazaro Mambosasa amelaani tukio hilo
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KUHUSU PICHA YA VIDEO INAYOSAMBAA MTANDAONI YA KUPIGWA MWANDISHI WA HABARI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linalaani vikali tukio linalosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandiishi wa habari wa WAPO Redio aitwaye SILLAS MBISE tukio lililotokea Tarehe 08.08.2018 siku ya mechi kati ya SIMBA vs ASANTE KOTOKO ya nchini Ghana, ambayo siku hiyo lilikuwa tukio la kuazimisha siku ya SIMBA(Simba day).
Aidha Polisi kanda maalum imeanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha ya video hiyo inayosambaa inayoonesha askari wa Polisi na mwandishi huyo wa habari ili kubaini ukweli.
Hiyo inaenda sambamba na kumtaka mtendewa wa kosa hilo la kupigwa kutoa taarifa kituo cha Polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. Kwani mtu yeyote anatakiwa kutoa malalamiko yake pale anapoona ametendewa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria.
Sambamba na hayo Polisi jukumu lake kuu ni kulinda usalama wa raia na mali zao na si kuwapiga raia walitenda kosa ambao hawajakataa kutii sheria ya kukamatwa.
L.B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
10.08.2018