Jina la Magufuli Labamba Uingereza: Ukumbi Mzima wa Chuo Kikuu cha Coventry Wazizima Baada ya Kusoma Jina la Muhitimu kutoka Tanzania.


Maprofesa wa Chuo Kikuu cha Coventry nchini Uingereza, wakiongozwa na Mkuu wa Chuo, Irene Glendinning, pamoja na Ukumbi mzima, ulizizima wakati jina la Mtanzania aitwaye Dk. John Pima lilipotajwa wakati wa Mahafali ya wahitimu wa Kozi ya Uzamivu wapatao 11 waliotoka katika Mataifa tisa duniani. 
Dk. Pima ambaye alikuwa shuhuda, alieleza kuwa, baada ya jina lake kusomwa ili aende mbele kutunukiwa shahada ya Uzamivu, walipotaja tu John Pima from Tanzania , shangwe ziliibuka wakitaja Magufuli .... Magufuli ... Magufuli ... Tanzania." 
Dk. Pima alieleza kuwa, baada ya mahafali, maprofesa na wahitimu wenzake walimfuata na kumuulizia habari za Rais Magufuli wanazosikia kwenye vyombo vya habari wakitaka kujua ni mtu wa namna gani? Wengi walipongeza kasi na msimamo wake wa: 
kukusanya mapato,kudhibiti matumizi ya fedha za umma,kushughulikia mafisadi,ununuzi wa ndege,upanuzi wa bandariujenzi wa barabara za juuuanzishwaji wa viwanda.

Walidai Nchi nyingi za kiafrika zina rasilimali nyingi lakini Viongozi wao hawana uthubutu wa kufanya maamuzi magumu na hawana maono kama ya Rais Magufuli, na kwamba hawatambui kuwa kama wanaweza kujiletea maendeleo pasipo kutegemea misaada kutoka mataifa makubwa.

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nilikutana na mtu wa South Africa nilipomwambia natoka tz akasema mna rais mzuri sana

    ReplyDelete
  2. "Gazeti lenyewe Uhuru", ulitaka Gazeti gani liandike? hata usipokubali sisi tunasonga mbele, Tanzania ya jana si ya leo, Hongera Rais wetu kwa kuthubutu na kuonesha njia ya kweli.

    ReplyDelete
  3. Nampenda magufuli rais wangu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad