JUKATA Yataka Wabunge Kuhama Vyama Na Ubunge Wao

Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema iko haja ya kuwapo kwa sheria ya kuruhusu wanasiasa kuhama vyama bila kupoteza nafasi zao za uongozi katika vyama wanavyohamia.

Mwenyekiti wa Jukata, Hebron Mwakagenda amesema hayo leo Jumatano Agosti 8, na kuongeza kuwa jukwaa hilo limefikia hatua hiyo baada ya kutafakari na kuona ipo haja ya kuruhusu mfumo huo ambapo pamoja na mambo mengine hatua hiyo itaokoa fedha za serikali katika kuendeleza nchi kihuduma na maendeleo.

“Kutokana na wimbi la wabunge na madiwani kuhama vyama kwa sababu mbalimbali na malalamiko ya Watanzania kuhusu gharama kubwa zinazotumika katika uchaguzi mdogo baada ya wanasiasa kuhama vyama.

“Kwa kuwa taifa linaingia katika kipinidi cha uchaguzi muda si mrefu ujao, Jukata tumetafakari na kuona ipo haja ya kuruhusu mfumo wa wanasiasa kuhama vyama pasipo kupoteza nafasi zao za kuchaguliwa,” amesema Mwakagenda.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad