Ramazani Shadari, Katibu Mtendaji wa chama kilichopo madarakani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) Jumatano ameteuliwa kuwa mgombea kiti cha urais kwenye uchaguzi wa Disemba 23, 2018.
Shadary anagombea nafasi hiyo kwa tiketi ya muungano wa vyama vinavyo tawala (FCC) nchini DRC.
Uteuzi huo umeondoa kitendawili kilichokuwepo kwamba huenda Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu 2001, angewania muhula mwengine.
Tayari Ramazani amewasilisha stakhabadhi zake za kuwania urais kwa tume ya ya uchaguzi jana mchana saa chache kabla ya muda uliowekwa kukamilika.
Emmanuel Shadari mwenye umri wa miaka 57 ni mwandani wa karibu wa rais Joseph kabila. Alikuwa katibu wa kudumu wa chama tawala cha PPRD na mtu muhimu wa kampeni za rais Kabila