Kabla ya Mwaka Kuisha Upimaji wa Tezi Dume Nyumba kwa Nyumba Utafanyika- Makonda

Kabla ya Mwaka Kuisha Upimaji wa Tezi Dume Nyumba kwa Nyumba Utafanyika- Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kabla ya mwaka huu kwisha, shughuli ya upimaji wa tezi dume itafanyika jijini humo.

Makonda ameyasema hayo leo Agosti 30, 2018 wakati akizundua kinga tiba ya magonjwa ya minyoo na kichocho kwa wanafunzi wa shule 708 za msingi za serikali na za binafsi za jiji hilo na wanafunzi 678,000 watapata chanjo hiyo.

Amesema mbali na magonjwa hayo kusababisha madhara kwa watoto lakini suala la upimaji wa tezi linashughulikiwa.

"Tunakamilisha utaratibu kabla ya mwaka huu tupite katika operesheni ya upimaji wa tezi dume," amesema Makonda na kuongeza:

"Wengi wanaamini tezi dume ni kwa ajili wanaume kumbe hata wanawake nao wapo."

Mkuu huyo wa mkoa ameendelea kuwasisitiza wakazi wa jiji hilo kuweka maeneo yao safi ili kujikinga na magonjwa yanayoepukika.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa huo, Grace Magembe amesema kinga hiyo itakuwa kati ya watoto wenye umri wa miaka 5-14 ambayo itatolewa shuleni na vituo vya afya kwa kipindi cha wiki mbili kuanzia sasa.

Amesema magonjwa ya kichocho husababisha ya saratani ya kibofu na tunawahamasisha wazazi na walezi kuhakikisha watoto wanapata kinga hii ambayo ni muhimu sana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad