KAKA wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), Alute Mughwai Lissu, amesema mwanaharakati Cyprian Musiba anapaswa kukamatwa na kushtakiwa kwa madai ya kwamba ametoa taarifa za uongo kwa umma kuhusu familia ya Lissu na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freema Mbowe.
Akizungumza na wanahabari, Mughwai amekanusha taarifa ya Musiba ambayo aliitoa hivi karibuni akisema amekutana na mke wa Lissu na kumweleza kwamba wamemzuia Mbowe kwenda kumjulia hali mgonjwa huko Ubelgiji anakotibiwa.
“Siwezi kumjibu Musiba, mtu wa hovyo, tangu lini amekutana na shemeji yangu akamwambia nimemkataza Mbowe kwenda kumuona mgonjwa? Tangu siku ya tukio mtu wa kwanza ambaye Tundu alisema aitwe ni Mbowe, amekuwa naye tangu Dodoma, na amekaa nsaye miezi mitatu Nairobi akimuuguza.
“Huu ni upuuzi, umeshawahi kumsikia huyo Musiba hata siku moja akisema amekwenda kumjulia hali Lissu? Kama watu wanakamatwa kila siku kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo, huyu Musiba anarokopa kila siku, anatakiwa naye akamatwe,” amesema Kaka wa Lissu.