Kala Jeremiah Azianika Mbinu za Kushinda Urais..Amtetea Nikki wa Pili na Ndoto yake ya Urais

Ikiwa imepita siku moja tokea rapa Nikki wa Pili kuzua gumzo mitandaoni juu ya ndoto yake ya kuwa na rais wa nchi hii na kupigwa vikali na watu mbalimbali, msanii Kalajeremiah ameibuka na kumshauri mwenzake kuwa asife moyo na maneno ya watu kwani ipo siku atatimiza lengo lake.



Kala Jeremiah ametoa ushauri huo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa instagram baada ya Nikki wa Pili kushambuliwa vikali kwa maneno juu ya jambo lake hilo, kwa kile kinachodaiwa kuwa hana sifa ya yeye kugombea nafasi kama hiyo kubwa huku wengine wakisema huenda ni kiki za wimbo wake mpya.

"Watu wengi hawajui maana ya ndoto, kwa hiyo wanamuangalia Nikki wa Pili kwa muonekano wa aliyo kuwa nao sasa, anafanya kazi gani, yuko karibu na nani na nani?. 'So' watu hawa wanakuweka moja kwa moja kwenye urais muda huu. Yani kwao ukisema una ndoto ya kuwa rais tafsiri yao ni kwamba unataka kuwa rais leo. watu hawa watakupinga tu",ameandika Kala Jeremiah.

Pamoja na hayo, Kala Jeremiah ameendelea kwa kusema kuwa
"watu wengi wanaogopa sana kuona mmoja kati yao anaendelea au ataendelea. Ukisema una ndoto ya kuwa rais watu waoga watakupinga sana kabisa maana wanajua mtu akisemacho kinaujaza moyo wake wanaamini utawazidi na hawataki uwazidi, huu uoga watu wengine wanauita wivu ila mimi naita uoga maana wivu ni ule wa kutaka maendeleo kama ya yule. Kwahiyo Nikk usijali kupingwa jali ndoto yako nami naamini itatimia. Weka mikakati songa mbele".

Mbali na hilo, Kala Jeremiah amempongeza rapa mwenzake kwa kuota ndoto kubwa na kudai imani siku zote inasema 'muota ndoto hafi kabla ya ndoto yake kutimia na kama muota ndoto hana imani na ndoto yake aweza kufa kabla ya kuitimiza'.

Mjadala wa kuwa Rais mara zote ukijitoka kutoka kwa watu ambao hawajafikiriwa au kudhaniwa kwa juu ya jambo hilo, siku zote huwa unazua mengi na kupelekea baadhi yao kuvunjika moyo kutokana na maneno ambayo ya ukatishwaji tamaa yaliyotolewa na watu fulani.

Rapa Kala Jeremiah pia yeye ni miongoni mwa wasanii waliowahi kujitangazia kuwa na lengo la kuja kuwa rais wa Tanzania hapo baadae, wakati alipokuwa anafanya mahojiano na chombo kimoja wapo cha habari lakini kwa bahati mbaya hakuweza kupata mapokezi mazuri kwa nyakati hizo na mwishowe akaambulia maneno ya kashfa na yenye kumkatisha tamaa.

EATV
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad