Kamati ya Maadili Yamfungia Maisha Kujihusisha na Soka Kigogo TFF

Kamati ya Maadili Yamfungia Maisha Kujihusisha na Soka Kigogo TFF
Kamati ya maadili ya Shirikishla Soka Tanzania (TFF) imemfungia maisha kutojihusisha na soka Mbasha Matutu.

Matutu ambaye ni Msimamizi wa kituo cha Shinyanga na Mjumbe wa Kamati kuu TFF, amefungiwa kwa kosa la kudanganya hesabu ya mapato kati ya mchezo wa Stand United na Simba SC.

Kiongozi huyo kwa sasa amefutwa rasmi wadhifa wake ndani ya Shirikisho hilo akiwa kama Mjumbe wa Kamati Kuu na sasa hatohusika tena na masuala ya soka nchini.

Maamuzi hayo yametolewa na TFF leo kupitia Makao yake yake yaliyopo Ilala, Karume baada ya kuitisha kikao na Waandishi wa Habari.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad