Kampuni ya Uber Kuanzisha Usafiri wa Boti Nchini

Kampuni ya Uber kuanzisha usafiri wa boti nchini
Kampuni ya huduma za usafiri inayotumia programu tumishi Uber imetangaza mpango wa kuanzisha huduma za boti Tanzania.

Kampuni hiyo kufikia sasa imekuwa ikitoa huduma za usafiri kupitia magari na bajaji.

Meneja masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki, Elizaberth Njeri amenukuliwa na gazeti la Mwananchi akisema huduma zilizopo za Uber zimefanikiwa vyema na ndio maana wakaamua kuanzisha pia huduma ya boti.

Kadhalika, Dar es Salaam ni mji wa pwani pamoja na visiwa vya Zanzibar na hivyo usafiri wa boti utafaa sana.

"Dar es Salaam imezungukwa na fukwe nzuri na visiwa vidogo vidogo lakini watu hawapati ladha halisi ya mandhari hayo kwa kuwa hawajui wanawezaje kufika huko. Huduma ya Uberboat ambayo inakaribia kuanza hivi karibuni itasaidia hilo," amesema Bi Njeri.

wiki mbili zijazo au mwezi mmoja lakini ndo hivi tumekwisha zindua. Hatutaishia Dar es Salaam na Zanzibar tu, tunatarajia kwenda na maeneo mengine kulingana na uhitaji wa soko."

Kampuni hiyo iliandaa tamasha kwa jina UberBOAT Party Jumamosi ambapo waliohudhuriwa walikuwa ni kwa mwaliko.

Kwenye app ya kampuni hiyo, kulikuwa na bango la kiungo cha UberBoat ambapo waliotaka kuhudhuria tamasha hiyo walitakiwa kukitumia kujiandikisha.

Uber imekuwa ikiendesha biashara barani Afrika kwa takriban miaka mitano sasa.

Kando na usafiri, kampuni hiyo imekuwa ikijihusisha katika biashara ya kusafirisha chakula kwa wakazi wa mijini ambapo wana huduma kama vile UberZenjiPizza ambayo ni huduma ya pizza ya Zanzibar na UberChoma ambayo ya nyama choma ikiwalenga wakazi wa Dar es Salaam.

Kampuni hiyo tayari ina huduma ya UberBoat katika maeneo mbalimbali duniani yakiwemo Croatia, Boston, Miami and Istanbul.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad