Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Nnauye ametoa neno baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi CUF Taifa, Julius Mtatiro kukihama chama hicho, akisema kuwa hamahama hiyo itumike kama fursa ya kujenga upya demokrasia.
Nape ametoa maneno hayo kupitia ukurasa wake wa Twitter, ambapo amesema hamahama hiyo pia itumike kama fursa ya kujenga uimara wa CCM.
Hata hivyo, Nape amesema uimara wa CCM unategemea ubora wa upinzani huku akifananisha na ushindani wa timu za Simba na Yanga.
"Kama msomi wa Sayansi ya siasa, naona hii ni FURSA muhimu ya KUJENGWA kwa aina MPYA ya VYAMA na SIASA za upinzani nchini! Kwa DEMOKRASIA hamahama hii ni muhimu ITUMIKE kama FURSA ya kujenga UPYA! Uimara wa CCM unategemea ubora wa UPINZANI!{Simba/Yanga} " ameandika Nape kupitia ukurasa wake wa Twitter.