MITANDAO ya kijamii hasa Instagram kwa sasa ndiyo habari ya mjini. Huku mastaa wanajiachia kwa kuweka mambo yao mbalimbali bila kusahau picha kali.
Kutokana na utamaduni huo wa kutupia picha kali kwenye mitandao ya kijamii kutawala kwa sasa, vijana wengi wamepata ajira kwa kushika kamera na kuwang’arisha mastaa.
Wapo wengi na hakika hawawezi kutosha kuwaelezea hapa. Lakini miongoni mwao ni Mingo ambaye anawapiga picha mastaa mbalimbali akiwemo Nay wa Mitego na Tunda. Kuna Bentiliya, mpiga picha wa Sanchoka, Hamisa Mobeto na mastaa mbalimbali na kuna Andrew Kisula ‘Kifesi’, aliyekuwa anawapiga picha mastaa kutoka Lebo ya Wasafi Classic Baby ‘WCB’ wakiongozwa na bosi wao Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’.
Mbali na kuwa mpiga picha tu Kifesi alijipatia umaarufu kwa picha zake kali ambazo zinatofautiana na wapiga picha wengi. Lakini siku za hivi karibuni tetesi ziliibuka kwenye mitandao ya kijamii na ikaelezwa kwamba amemwagana na WCB, Ijumaa likaamua kumsaka na huyu hapa anafunguka mambo mengi:
Picha inayohusiana
IJUMAA: Niaje Kifesi?
KIFESI: Poa, inakuwaje?
IJUMAA: Haiwi kitu. Tuanzie kwenye jina lako la Kifesi, lilitokana na nini?
KIFESI: Nilianza kuitwa kiutani na kina Moses Iyobo, kwa sababu baba yangu alikuwa anaitwa Kisula na wao wakaunga juu kwa juu.
IJUMAA: Wewe ni miongoni mwa wapiga picha Bongo wenye elimu, unaweza kuwaeleza wasomaji wetu juu ya elimu yako?
KIFESI: Nina Diploma kwenye masuala ya uhusiano.
IJUMAA: Mbali na kupiga picha kuna shughuli nyingine unafanya?
KIFESI: Hapana. Kwa sasa hiyo ndiyo shughuli yangu kuu. Lakini pia ninamiliki studio ya kupigia picha ingawa pia kuna mipango ya kuanzisha biashara ya chakula na kuendesha kipindi cha mahusiano kitakachorushwa kwenye televisheni.
IJUMAA: Kuna tetesi kwamba umezinguana na uongozi wa WCB, nini sababu hasa?
KIFESI: Hakuna zaidi, ila nimeamua kukaa pembeni. Si unajua kuna muda unafika na unahitaji kusimama wewe kama wewe!
IJUMAA: Siyo kwamba kuna ishu chini ya pazia?
KIFESI: Hakuna lolote. Ni mimi mwenyewe tu nimeamua kujitegemea.
IJUMAA: Ukiwa WCB, ulikuwa unakutana na changamoto gani?
KIFESI: Ambacho kilikuwa kinanikwaza ilikuwa ni kufanya kazi mpaka siku zangu za ibada, hili lilikuwa linanichukiza sana maana
nilijikuta nikiishi maisha ambayo siyo yangu. Namshukuru Mungu kwa sasa ninajitegemea mwenyewe.
IJUMAA: Vipi kuhusu faida?
KIFESI: Kutambulika kwa watu wengi.
IJUMAA: Kuna tofauti gani kwa sasa, ulipo kuwa pale WCB na unavyojitegemea?
KIFESI: Kwa sasa nina uhuru, amani na ninafanya kazi bila kusimamiwa na mtu yeyote. Lakini pia kipato changu kimeongezeka kulingana na kwamba ninafanya kazi kwa wingi niwezavyo.
IJUMAA: Bado una mawasiliano na Diamond?
KIFESI: Siwasiliani naye, ‘aliniblock’, lakini binafsi bado ninamheshimu, nina mthamini na ninamchukulia kama mtu mwenye mchango kwangu mkubwa.
IJUMAA: Vipi kuhusu Zari, bado unawasiliana naye?
KIFESI: Ndiyo, Zari ni rafiki yangu na tunaheshimiana.
IJUMAA: Ukiambiwa leo urudi WCB utakubali?
KIFESI: Hapana. Ninafurahia maisha yangu ninayoishi sasa kwa hiyo sijawaza kabisa juu ya jambo hilo na siwezi.
IJUMAA: Una kipi cha kumalizia?
KIFESI: Mungu ni mkubwa kwenye kazi zangu na ninamthamini sana na ninawakubali wote wanaonipa sapoti.
Kifesi Afunguka Ukaribu Wake na Zari Atoboa Siri ya Daimond Alivyomblock
0
August 03, 2018
Tags