Akizungumza na www.eatv.tv hii leo Joh Makini amesema tuzo ilikuwa inampa hamasa msanii kwa kuendelee kuumiza kichwa, juu ya kutoa ngoma kali kusudi aweze kuingia kwenye kinyang'anyiro hicho cha tuzo.
"Tuzo ni kitu cha msingi na kipimo tosha kwa msanii kuwa ana uwezo kiasi gani ila kwa sisi Weusi, tunajua nini tunafanya na tunaamini ni wakali ndio maana huwa tunafanya vitu vingi ambavyo vinawashangaza watu", amesema Joh Makini.
Aidha, Joh Makini amesema msanii ni mfano wa mwanafunzi ambaye yupo shuleni kwa lengo la kusoma kwa bidii na kuweza kushika nafasi ya kwanza au pili, kusudi mtu huyo apate zawadi fulani au sifa nzuri nyumbani kwao au kwa majama zake kwa kile alichokifanya.
Mbali na hilo, Joh Makini amesema sababu kubwa ya wasanii wa hiphop kushindwa kufanya vizuri, ni kutokana na mipaka waliyojiwekea wakati sanaa wanayoitumikia haipo hivyo, huku akimtolea mfano 'role model' wake Jay Z kuwa kila siku anabadilika na kuwa mpya kutokana na mahitaji ya mashabiki zake wanavyotaka na soko kiujumla.
EATV