Kitendawili cha jezi Mpya za Yanga


NA ELBOGAST MYALUKO
Pamoja na kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu soka Tanzania Bara msimu wa 2018/19, Yanga imebainisha kuwa bado haijawa na jezi mpya rasmi kwaajili ya msimu wa mashindano wa 2018/19 kitu ambacho si kawaida kwa timu kubwa.

 Kupitia taarifa yake, Yanga imethibitisha kuwa kama klabu haijatengeneza jezi mpya kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao hivyo bado wanatumia jezi zilezile za msimu uliopita katika mechi zao.

''Ifahamike kuwa bado hatujatangaza jezi mpya hivyo popote usikubali kununua jezi kwa kisingizio cha jezi mpya ya Yanga'', imeeleza taarifa.

Yanga imefafanua kuwa ipo kwenye mikakati ya kuhakikisha inakamilisha upatikanaji wa jezi mpya kwaajili ya mashindano yote msimu ya msimu huu ambapo itashiriki katika michuano mbalimbali ikiwemo ligi kuu na kombe la shirikisho nchini.

Yanga ilipitia changamoto ya kulazimika kutumia jezi zisizo na nembo ya mdhamini, kwenye mechi yao ya kwanza ya makundi kombe la shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger mwezi Mei mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad