LICHA ya kutoweka wazi juu ya mchakato wa ndani ulivyo lakini habari ni kuwa Kocha Jose Mourinho amekasirishwa na kitendo cha uongozi wa timu yake ya Manchester United kushindwa kumpatia fedha za usajili alizohitaji.
Dirisha la usajili lilifungwa juzi Alhamisi na kocha huyo bado alikuwa na matumaini ya kufanya usajili hasa wa beki wa kati, baada ya kukwama kote akataka kumsajili mkongwe wa Atletico Madrid, Diego Godin kwa pauni 18m lakini beki huyo akaamua kuendelea kubaki Hispania.
Licha ya kuzungumza na waandishi wa habari juzi akiwa na utulivu, habari za ndani zinaeleza kuwa kocha huyo alikuwa na hasira kali kabla ya mchezo wa jana ambapo timu yake ilicheza dhidi ya Leicester City kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Mourinho alikuwa tayari kutumia hata pauni milioni 100 kufanya usajili wa beki wa kati lakini hilo lilipingwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu, Ed Woodward. “Najua maneno mnayotaka niseme lakini
siwezi kusema chochote,” alisema Mourinho kabla ya kuivaa Leicester mara baada ya kuhojiwa na waandishi wa habari.
Kocha huyo amesema mashabiki wasubiri kuona Novemba au Desemba kuona mwelekeo wa timu yao utakuwaje. Mourinho alihitaji wachezaji watano baada ya msimu uliopita kumalizika lakini hadi dakika za mwisho akawa anahitaji angalau wawili lakini nao hakuwapata. Ndani ya miaka miwili aliyodumu klabuni hapo, kocha huyo ameshatumia pauni milioni 375 kwa ajili ya usajili.
Kocha Jose MourinhoAtibuana na Uongozi wa Manchester United
0
August 11, 2018
Tags