Kwa Hili Paul Makonda yupo sahihi, Waziri Embu Angalia cha Kufanya


Swala hapa ni vifaa kwa ajiri ya kusaidia elimu ya Dar es Salaam ambayo ina changamoto nyingi ikiwa na mrundikano wa wanafunzi na mambo kibao

Makonda inawezekana kuna sehemu alikosea katika mchakato huo lakini serikali walitakiwa kuwa wajanja wangeruhusu kwanza vitu viingie ndio waanze kuvimonitor wapate ushahidi wa kutosha ndio waje kumtuhumu.

matokeo yake wananchi nao wameyabeba na kusahau watoto wao ndio wanakaa chini milele
mimi niko na ushahidi kabisa nilienda shule moja na taasisi fulani kutoa msaada wa computer lakini unakuta walimu stafu viti tu vya kukalia haviwatoshi hii ni aibu kama mwalimu hana kiti stafu mwanafunzi je darasani itakuwaje?

tukiweka siasa pembeni Makonda yupo sahihi kabisa na ana nia njema ingawa anaweza kuwa kafanya makosa kutumia jina lake kwa ushauri mbovu wa watendaji waliopo chini yake lakini naamini tatizo letu la elimu ni kubwa mno kuliko jina la makonda kuwa kwenye makontenana hili swala tunalibabe kishabiki sana kama kawaida yetu...

kwamba mimi ni chadema Gambo akifiwa na mzazi wake nashangilia, mimi ni ccm Sugu akipata msiba nashangilia upuuzi mtupu.

Hivi waziri anavipiga mnada vitu vya shule za Dar es Salaam watu tunashangilia leo halafu kesho Jangwani Secondary inakuwa ya mwisho tunaanza kumponda Paul Makonda ...

Hivi vitu vikinunuliwa na wafanya biashara sisi wananchi wa kawaida tutafaidika vipi direct kama ambavyo tungeviona kwenye shule zetu?

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad