Lemutuz Atoa Mpya..Amtaka Rich Mavoko Ajirudi na Kuwaomba Msamaha WCB


Mdau wa mambo ya sanaa na mwanasiasa William Malecela maarufu Kwenye mitandao ya kijamii kama Lemutuz amemfungukia Rich Mavoko na kumtaka amalize mgogoro wake na iliyokuwa Label yake WCB.

Wiki iliyopita Rich Mavoko aliwaburuza WCB, Baraza la sanaa Tanzania (BASATA) kwa madai ya mikataba mibovu ambayo amedai imemnyonya na kutompa maslahi ya kufaa.

Baada ya sakata hilo Lemutuz amepima uzito suala hilo na kumshauri Rich Mavoko arudi WCB awaombe msamaha ili asiondoke kwa shari kwani hajui kesho yake ikoje.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Lemutuz ameandika:

FACT: BAADA YA KUONA KELELE NYINGI HUMU INSTAGRAM MY OPINION….Ni kijana mdogo ambaye ninakuheshimu sana U know that ….sijui yaliyojiri humo ndani ila UNAKOSEA SANA KUONDOKA KWA VITA ….it is WRONG ….MKATABA MBOVU HAUTATULIWI INSTAGRAM……Qboy alipofikia ulipofikia ni mimi niliyemshauri kuondoka kwa amani hata kama wamekufanyia ubaya gani ONDOKA KWA AMANI cause kuna mazuri waliyokufanyia yahesabu uyashikilie …..ni kawaida ya sisi masikini kushangilia vita ya masikini mwenzetu na Tajiri tukiamini huenda utamuangusha Tajiri… ila ni kwa muda mfupi sana then wote sisi masikini tunarudi kwa Tajri wewe tunakusahau …HUJACHELEWA TAFUTA NJIA UYAWEKE SAWA NAO ….USEPE …nina tatizo na binadam yoyote asiyekuwa na Shukrani na anayevunja madaraja aliyoyapitia kufikia alipofikia sasa …ni mimi niliyemshauri Mwarabu sasa anafungua kampuni yake bila vita na alikotoka …Kijana mdogo waombe radhi Wasafi ili muchane kwa amani ….NI USHAURI WA BURE TU uchukue au niachie! …ila ninakupa kwa nia njema sana! …… @lemutuz_superbrand

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad