Madee amesema hayo kupitia akaunti yake ya Instagram huku akimuombea apone haraka ili aweze kuendelea kufanya kazi zake.
"Kwenye maombi yetu yakila siku tusimsahau Omary.. ... tumuombee apone haraka aendelee na majukumu yake ,Omary anaumwa .. tuseme Ameeeen🙏🙏," ameandika Madee kwenye mtandao huo.
Ni mwezi wa tatu sasa tangu Ommy Dimpoz atangaze kuwa amefanyiwa upasuaji wa koromeo, hata hivyo bado hakuna taarifa rasmi zilizotolewa na uongozi wake juu ya maendeleo ya afya yake.