Madeni yamvuruga Msemaji wa Serikali


Serikali imesema kuwa iko kwenye mchakato wa kuunda mfumo madhubuti wa kutoa matangazo yake na taasisi zake katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abasi, alipokuwa akizungumza na wahariri na waandishi wa habari wa New Habari (2006) Ltd.

Amesema hatua hiyo inatokana na changamoto iliyogusa biashara ya matangazo serikalini na kuongeza kuwa amekuta barua nyingi za vyombo vya habari zikidai madeni yao yanayotokana na matangazo.

“Ni madeni ambayo serikali inadaiwa kwa kutangaza, Vyombo vya habari karibu vyote vinaidai serikali, nafikiri hata wahariri kwenye moja ya tamko lao walilisema hilo lakini waliliweka kwenye namna ambayo asiyeelewa hawezi kuelewa, lakini tulioelewa tulielewa,”amesema Dkt. Abbas

Aidha, Dkt. Abbas ameongeza kuwa biashara hiyo ilikuwa holela holela, kwa hiyo amekuta mafaili na barua za watu waliokuwa wakikubaliana kienyeji na kutangaza huku shughuli ikibaki kwenye malipo

Hata hivyo, amesema kuwa kama kuna kesi kubwa zinazochangia hali mbaya kwa vyombo vya habari ni hiyo hali kwamba watu waliingia mikataba ya kutangaza hayo matangazo ambapo yule ofisa anayeingia naye alikuwa anaiwahi hiyo asilimia 10 (commission) ya matangazo hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad