Mafanikio ya Zidane njaa Kwa Makocha Vijana Waliotoka Viwanjani, Je Wataweza Kumfikia?

Wakati Zinedine Zidane anaiongoza Real Madrid kutwaa taji la tatu barani Ulaya, likiwa taji lake la tatu mfululizo hakuwa peke yake katika kushangilia mafanikio hayo makubwa. Ndiyo hakuwa pekeake kwani mafanikio yale yaliwahusu makocha vijana waliowahi kujijengea majina kama wachezaji na leo wamegeukia ukocha katika mazingira magumu kuliko yale waliyokuwanayo kama wachezaji.



Ushindi wa Zidane ulipokewa kwa furaha na makocha wachanga wanaochipukia kwani inawapa imani kuwa, kukosa uzoefu sio kigezo cha kukosa nafasi katika tasnia ya ukocha.

Usiku wa jana Frank Lampard alianza rasmi maisha ya kiushindani kama kocha wa Derby County inayoshiriki ligi daraja la pili England ligi inayofahamika kama Championship.



Wakati Super Frankie anaikabiri Reading jana, Jumapili swahiba wake Stiven Gerrard ambaye walicheza pamoja katika nafasi ya kiungo kwenye timu ya taifa ya England ataiongoza Rangers kwenye ligi ya Scotland kwa mara ya kwanza akiwa tayari ameivusha timu hiyo kwenye hatua mbili za michuano ya Europa.

Lampard na Gerrard hawapo pekeyao kwenye hili, kwani nchini Ufaransa kiungo mwingine akiyewika England Patrick Vieira naye atakuwa anaanza maisha mapya kama kocha kwenye ligi kubwa kwenye timu ya Nice kama ilivyo kwa Joey Barton ambaye amepewa timu ya Fleetwood Town inayoshiriki ligi daraja la tatu England bila kumsahau Michael Carrick ambaye ameteuliwa kuwa msaidizi wa Jose Mourinho.



Mazingira wanayojikuta nayo viungo hawa wa zamani leo hii wakiwa makocha ni tofauti sana na ilivyokuwa enzi zao wakati wa nakipiga. Enzi za uchezaji wao viungo hawa kwa nyakati tofauti walichezea timu kubwa wakiziongoza kupata mafanikio ya ndani na hata nje ya kimataifa.

Hakuna anayehitaji kukumbushwa Arsenal ilinoga kiasi gani wakati Viera akitawala dimba ama ubora wa Gerrard usiku ule Liverpool walipoiteka Ulaya pale Istanbul au historia ya ufungaji bora kwenye historia ya Chelsea aliyonayo Frank Lampard achiliambali vurugu za Joey Barton akiwa Man City na baadae Newcastle na Carrick alipokuwa kwenye kilele cha kipaji chake akiiongoza United kutwaa mataji sita ya EPL.



Maisha ya ukocha hayatakuwa eneo la kujidai kama ilivyokuwa wakati wanacheza, huku watakutana na matusi ya mashabiki, presha za viongozi bila kusahau maoni ya wachezaji wenzao wa zamani ambao wengi ni wachambuzi na hawatasita kuwaponda wenzao pale watakapokuwa ofisini mbele ya camera za television kwenye matangazo ya mechi kila weekend.

Gary Naville alikutana na joto ya jiwe katika muda mfupi aliozama kwenye ukocha akiwa na Valensia na matokeo yake yalimvunja moyo kiasi cha kutotamani kurudi tena kwenye benchi. Watu kama Mourinho walimkaribisha kwa vijembe wakikumbushia maneno anayotumia kwenye uchambuzi dhidi yao na hawakuiacha naasi ya kumlipizia.

Hata hivyo mafanikio ya Zidane pamoja na imani ya Madrid ambayo iliwekeza kwake ni ushahidi tosha kwamba makocha hawa wapya wakiaminiwa wanaweza kufanya kitu cha ujasiri wa kuweza kushuka madaraja ya chini na sehemu walipokuwa wanacheza inaonesha uvumilivu walio tayari kuwa nao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad