Mahakama Mfawidhi Iringa Yamkuta na Kesi ya Kujibu Abdul Nondo

Mahakama Mfawidhi Iringa Yamkuta na Kesi ya Kujibu Abdul Nondo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Iringa imeamua kuwa Mwenyekiti wa mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo  ana kesi ya kujibu katika mashtaka yote mawili yanayomkabili ikiwemo.


Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa 'WhatsApp' kuwa yupo hatarini, kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi wa kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.

Baada ya mahakama kutoa umamuzi huo leo  Agosti 27, 2018 mshtakiwa Nondo  atawatumia mashahidi watano kujitetea na kesi hiyo itasikilizwa tarehe 18 na 19 mwezi ujao.

Awali Mahakama ilishindwa kuendelea kusikiliza ushahidi wa mashahidi wawili kati ya watano wa kesi hiyo baada mshitakiwa kuiandikia barua Mahakama  akimtaka Hakimu John Mpitanjia anayesikiliza kesi yake ajitoe kwa sababu ya kupoteza imani naye.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad