Mahakama ya Kikatiba Yaidhinisha Ushindi wa Emmersom Mnangagwa Zimbabwe

Mahakama ya kikatiba yaidhinisha ushindi wa Emmersom Mnangagwa Zimbabwe
Ushindi wa Rais Emmerson Mnangagwa kwenye uchaguzi wa mwezi uliopita umeidhinishwa na mahakama ya kikatiba ya nchi hiyo.

Chama cha upinzani cha MDC kilikuwa kimepeleka kesi mahakamani kupinga, kikisema uchaguzi huo ulikumbwa na dosari lakini hilo limekataliwa na mahakama.

Akisoma uamuzi huo Jaji Mkuu Luke Malaba alitaja madai hayo kuwa yasiyo ya ukweli.

Ndio uchaguzi wa kwanza nchini humo tangu kiongozi wa miaka mingi Robert Mugabe aondelewe madarakani mwaka uliopita.

Siku mbili baada ya uchaguzi takriban watu 6 waliuawa kwenye ghasia kati ya jeshi na wafuasi wa Muungano wa MDC ambao wanadai kuwa kiongozi wao Nelson Chamisa alikuwa ameibiwa ushindi.


Kabla ya kutolewa uamuzi huo mitaa inayozunguka mahakama kwenye mji mkuu Harare ilifungwa na vikosi vya usalama.


Kwenye uamuzi huo wa pamoja majaji tisa waliamua kuwa kesi ya upinzani haikuwa na ushahidi wa kutosha.

"Ushahidi mzuri ungekuwa kile kilicho kwenye masanduku ya kupigia kura," jaji mkuu Malab alisema.

Rais Emmerson Mnangagwa alinusurika duru ya pili wakati aliibuka mshindi kwa asilimia 50.7.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad