Maimatha Ambwaga Zari Ahamisha Majeshi kwa Hamisa Mobetto

Mwanadada Maiamartha wa Jesse ambae amejipatia umaaarufu sana kwa kupitia kazi yake ya utangazaji na sasa hivi ni MC amejikuta akihamisha majeshi na mapenzi aliyokuwa nayo kwa mwanamama Zari kutoka Uganda na kuanza kumpenda na kumpalilia Hamisa mobeto kutoka Tanzania .

Kwa hali isiyo ya kawaida mwanadada Maimartha alikuwa akimsifia sana Zari hapo awali  na alishawahi mpaka kumwambai hamisa kuwa ajiengue katika kuweka bifu na Zari kwa sababu Zari sio saizi yake na wala hana haja ya kuwa akigombana nae sana katika mitandao kwa sababu ya mwanaume.

Hata hivyo , Maimartha alianza kuonekana akihama upande huo taratibu na hata kufikia hatua ya kusema kuwa Zari ana roho mbaya baada ya  kusikika kuwa Zari alikataa kuwakaribisha nyumbani kwao kwa ajili ya sherehe ya mtoto wao.

Baada ya Hamisa kutoa wimbo wake hivi karibuni, Maimartha kupitia katika ukurasa wake aliweka post ya kumpongeza hamisa kwa kuandika “Hamisa…Go girl i feel hot..” baada ya Hamisa kutoa wimbo wake wa madam Hero.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad