Maisha:Inakugharimu Kiasi Gani Kuyafanya Haya Kwa Watu?



1. Inakugharimu kiasi gani kumsalimia Mlinzi anaekufungulia geti ukiingia kazini/nyumbani?
-
2. Je, inakugharimu kiasi gani kumuomba mfanya usafi akuruhusu upite kuliko kukanyaga mahali alipodeki na hapajakauka bado?
-
3. Ndugu, inakugharimu kiasi gani kumshukuru mtu aliyekutendea wema?
-
4. Hivi, inakugharimu kiasi gani kumpakulia Mkeo chakula baada ya yeye kupika?
-
5. Je, inakugharimu kiasi gani kumsalimia na kumtendea vyema mtu usiemjua?
-
Mdau wetu, ni mambo yapi mema unadhani ni vyema kuwakumbusha watu kuyatenda?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad