Maiti za wanawake wanne Mwanza Zakutwa Zimenyofolewa Viungo


MWANZA: Maiti za wanawake wanne kutoka vijiji vya Misasi, Isakamawe na Mabuki wilayani Misungwi zimepatikana huku zikiwa hazina baadhi ya viungo
-
Miili hiyo imeokotwa maeneo tofauti ikiwa na alama zinazoonyesha walinyongwa kabla ya kufariki.
-
John Makoye mkazi wa Isakamawe aliyeshuhudia maiti ya marehemu hao ametaja baadhi ya viungo vilivyonyofolewa kuwa ni ulimi, matiti na sehemu ya siri.
-
Aidha, Kamanda wa Polisi, Ahmed Msangi amewataja waliouawa kuwa ni Angelina Lumala(45) mkazi wa Isakamawe, Kundi Laurent(35) na Mariamu Manila(30) wakazi wa Misasi na mmoja aliyetambulika kwa jina la Ngole(43) mkazi wa Kitongoji cha Bujingwa kijiji cha Mabuki.
-
Amesema Polisi tayari inawashikilia kwa mahojiano watu watatu ambao hakuwa tayari kuwataja majina waliokutwa kwenye mapori ambako miili hiyo ilikutwa
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad