Makampuni Yanayotoa Huduma za Internet Yaagizwa Kufungia Tovuti za Picha Chafu ‘Pornography’ Ifikapo Mwezi Septemba 2018

Makampuni yanayotoa huduma za Internet yaagizwa kufungia tovuti za picha chafu ‘Pornography’ ifikapo mwezi Septemba 2018
Kwa kile kinachoonekana ni kulinda maadili ya wananchi nchini Uganda, Serikali ya nchi hiyo kupitia Mamlaka ya Mawasiliano nchini humo (UCC) imeyatangazia makampuni yanayojihusisha na utoaji wa huduma ya Internet (Internet Service Providers- ISPs) na Mitandao ya simu kufungia tovuti zinazorusha picha chafu.

Mkurugenzi Mtendaji wa UCC, Godfrey Mutabazi amesema kuwa nchini Uganda kuna tovuti 17 ndani ya nchi hiyo ambazo zinatoa huduma hiyo huku tovuti 10 za kimataifa zikiwa zinaongoza kutazamwa ambapo amedai kuwa ameshaagiza makampuni yote tajwa yafungie mitandao hiyo kabla ya mwezi Septemba mwaka huu.

“Mamlaka yetu imebaini kuwa kuna tovuti nyingi nchini zinazoonesha picha chafu, hii ni kutokana na Kamati yetu ya Kudhibiti Masuala ya Ngono Mtandaoni. Kamati hiyo pia imebaini kuwa kuna tovuti za ngono ambazo zinaonesha mubashara kiyu ambacho kinavunja sheria moja moja ya nchi ya kifungu namba 13 cha sheria ya mwaka 2014 inayokataza masuala ya picha chafu.“amesema Robert Mutabazi kwenye mahojiano yake na UBC.

Sakata hilo la kubaini tovuti zinazoonesha picha chafu lilianza mwaka 2016 baada ya nchi hiyo kununua kifaa maalumu (Pornography-Detecting Machine) cha kubaini tovuti zinazorusha Ponografia nchini humo.

Mutabazi amesema kuwa makampuni ambayo yatakiuka agizo hilo hadi kufikia mwezi Septemba 2018 yatatozwa faini.

Hayo yote yanajiri ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu taifa hilo lipitishe sheria ya kutoza kodi kwa watumiaji wote wa mitandao ya kijamii.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad