MAKAMU rais wa zamani wa shirikisho la soka duniani (FIFA) amehukumiwa kifungo cha miaka tisa nchini Marekani ikiwa ni matokeo ya uchunguzi wa rushwa iliyofanywa ndani ya chombo hicho kikubwa cha soka duniani.
Juan Angel Napout, ambaye anatokea Paraguay alipatikana na hatia ya kuchukua mamilioni ya dola kwa njia ya rushwa.
Hatua hii inakuja siku chache baada ya kifungo cha miaka minne alichopewa mkuu wa zamani wa soka nchini Brazil, Jose Maria Marin, ambaye pia alihusishwa kwenye tuhuma hizohizo. Wote kwa pamoja walikutwa na hatia ya kupokea rushwa kutoka makampuni makubwa ambayo yalikuwa yakijitangaza kupitia FIFA.