Mamaake Osama Bin Laden Amkumbuka Mwanaye Asema Alikua 'Mtoto Mzuri'

Mamake Osama Bin Laden Amkumbuka Mwanaye Asema Alikua 'Mtoto Mzuri'
Mamake kiongozi wa al-Qaeda Osama Bin Laden amezungumza hadharani kwa mara ya kwanza , miaka saba baada ya kifo cha mwanawe mwaka 2011.

Alia Ghanem alifanya mahojiano na gazeti la The Guradian katika nyumba ya familia hiyo mjini Jeddah Saudia.

Aliambia gazeti hilo kwamba ,mwanawe alikuwa mwenye haya na mtoto mzuri lakini akapewa itikadi mbaya akiwa chuo kikuu.

Familia hiyo inasema kwamba mara ya mwisho kumuona Bin Laden ilikuwa 1999, miaka miwili kabla ya mashambulio wakati alipokuwa akiishi nchini Afghanistan.

Moise Katumbi akwama katika mpaka wa DR Congo
Wakati alipogunduliwa kuwa mshukiwa mkuu wa ugaidi duniani, baada ya kuhamia nchini humo ili kupigana dhidi ya vikosi vya Sovieti vilivyovamia 1980.

''Tulikasirika sana , sikutaka matatizo hayo kutokea, kwa nini alibadilika na kuwa namna hiyo mara moja''? Bi Ghanem aliambia gazeti hilo, alipoulizwa alihisi vipi alipogundua kwamba mwanawe amebadilika na kuwa mpiganaji wa kijihadi.

Pia alisema kuwa kundi la Muslim Brotherhood ambalo mwanawe alihusika nalo wakati wa masomo lilikuwa kama madhehebu.

Mtoto mwenye siku 12 ang'olewa jino
Familia ya Bin Laden imesalia kuwa familia maarufu zaidi nchini Saudia baada ya kujipatia utajiri mkubwa kupitia ujenzi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad