Mapigano Yatokea Kisalawe na Mkuranga

Mapigano Yatokea Kisalawe na Mkuranga
Mkuu wa Wilaya ya Mkurannga Mh. Filberto Sanga amethibitisha kutokea kwa mapigano mapema leo baina ya wafugaji na wakulima ambayo yamesababisha kujeruhiwa kwa watu zaidi ya watano mpakani mwa Wilaya hiyo na wilaya ya Kisarawe.

Sanga, amesema katika majeruhi hao mmoja hali yake ni mbaya na amesafirishwa kuelekea Hospitali ya taifa ya Mhimbili kwa matibabu zaidi huku akisema baadhi ya watu waliojeruhiwa ni wakazi wa Dar es Salaam wanaofanya shughuli za kilimo wilayani humo.

Mapigano hayo yametokea katika kijiji cha Kondomwelanzi kata ya Bupu ambapo diwani wa kata hiyo Bw. Abasi Msangule amesema mapigano yametokea baada ya kundi la wafugaji jamii ya Kimang'ati kuingiza kwa nguvu mifugo yako katika mashamba ya wakulima.

Bw. Msangule, ameongeza kuwa baada ya kuona mapigano hayo alichukua hatua ya kuwasiliana na uongozi wa wilaya ya Mkuranga ambapo walifika eneo la tukio na kukuta tayari watu sita wameshajeruhiwa wengi wao wakiwa ni wa upande wa wakulima.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad