Jeshi la Majini la Marekani limepeleka manowari yake ya kivita, 2nd Fleet, kwaajili ya kuimarisha ulinzi upande wa Kaskazini mwa bahari ya Atlantic ambapo jeshi la Urusi linafanya operesheni za kivita katika kasi ambayo haijawahi kushuhudiwa tangu kumalizika kwa Vita Baridi vya Dunia.
Mabadiliko hayo kwa sehemu kubwa ni ya kiutawala na yamemrudisha msimamizi mwenye cheo cha admiral atakaye husika kusimamia manowari za kivita zote za Marekani wakati zikiendelea kulinda eneo kati ya Pwani ya Mashariki ya Marekani na Bahari ya Barents, iliyoko nje ya pwani ya Norway na Urusi.
Aidha, kurudishwa kwa manowari hiyo inaonyesha kuwa kuna mabadiliko makubwa katika mkakati wa jeshi la Marekani, ambapo jambo la msingi linalozingatiwa ni kuhama kutoka katika vita ya ugaidi, Mashariki ya Kati, na kuangalia ushindani unaozidi kupamba moto kati yake na Urusi na China.
“Sisi hatutaki vita lakini kinachofanyika ni kuweza kujilinda kwa nguvu zote na uwezo wa hali ya juu ili kuweza kukabliana na chochote kile,”amesema Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Majini, John Richardson akiwa katika manowari ya kivita USS George H. W. Bush inayobeba ndege za kivita huko Norfolk, Virginia
Barabara ya chini ya Ardhi ya kusafirisha dawa za kulevya yagundulika
Hata hivyo, Richardson ameongeza kuwa kama itahitajika manowari ya 2nd Fleet itafanya mashambulizi yeyote yatakayohitajika ili kuweza kukabiliana na adui yeyote.