Mashekhe na Mapadri Wameniombea Imeshindikana, Watanzania Nichangieni na Mimi Nizae – Diva

Mashekhe na Mapadri wameniombea imeshindikana, Watanzania nichangieni na mimi nizae – Diva
Wakati kuna wanawake wanatupa vichanga majararani bila hata hofu ya Mungu, upande mwingine wapo wanawake ambao wanahangaika kila uchwao kutafuta watoto kwa udi na uvumba.



Mfano wa Wanawake hao ni Mtangazaji wa kituo cha Radio cha Clouds FM ambaye amekiri wazi kuwa amehangaika kwa kipindi kirefu kutafuta mtoto lakini imekuwa ikishindikana kumpata.

Akielezea safari hiyo, Diva amedai kuwa ameombewa na Mashekhe  na Mapadri na kunywa kila aina ya dawa ya uzazi lakini hajafanikiwa hadi alipopewa majibu na wataalamu kuwa mirija ya uzazi imeharibika hivyo hataweza kuzaa kwa njia ya kawaida.

Diva kwa sasa anawaomba Watanzania wamsaidie kwa kumchangia kiasi cha dola $7,000 ambacho ni zaidi ya Milioni 15 ili aweze kwenda Marekani kwa ajili ya IVF Treatments yaani mfumo wa kupandikizwa mbegu za kiume.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bongo kweli vyuma vimekaza mpaka akina Diva anaomba achangiwe sio kwamba anataka achangiwe ili aweze kupata mimba huyo anataka achangiwe hela ya kumudu maisha

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad