Masikini! Waziri Kigwangala Asheherekea Siku Yake ya Kuzaliwa Akiwa Hospitalini..... Atoa Hisia Zake kwa Uchungu

Masikini! Waziri Kigwangala Asheherekea Siku Yake ya Kuzaliwa Akiwa Hospitalini..... Atoa Hisia Zake kwa Uchungu
Ikiwa siku chache zimepita baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Hamis Kigwangala kupata ajali lakini  leo anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili anakotibiwa.

Dk Kigwangala, leo Agosti 7, anatimiza miaka 43 ya kuzaliwa kwake.

Ameandika katika ukurasa wake wa twitter akimshukuru Mungu kwa kufikisha umri huyo.

''Its my 43rd birthday today, alhamdulillah. Ahsante Allah kwa kunifikisha leo hii. Mimi ni shuhuda wa nguvu zako na upendo wako. Hakika wewe ni Mkuu, ni mwema sana. Ni mwenye huruma sana. Ni mwenye kusamehe sana. Ni mwenye kurehemu neema kubwa kubwa na neema ndogo ndogo. Umenipa mtihani na funzo kubwa sana kwenye maisha yangu. Naomba uendelee kunipa ulinzi wako. Unijaalie maisha mema marefu yenye faida kwangu na kwa viumbe wako. Nakushukuru kwa hali hii na ninajua utaniafu mapema ili nizidi kuutangaza ukuu na utukufu wako ya Allah. Kwa uamuzi na kwa uweza wako hakuna kinachoshindikana ya Allah. Wewe ndiyo kila kitu. Ninakuomba siha, furaha na mafanikio tele kwa familia yangu, ndugu, jamaa, viongozi wakuu wangu, viongozi wenzangu, marafiki na wananchi wenzangu wote wanaoniombea dua. Kwa wapiga kura wenzangu wa Nzega, poleni, nilikuwa nakuja ziara yetu ya jimbo ndo nikapata ajali hii; mzidi kuniombea dua ili nipone haraka niendelee kuwatumikia. Kwa sasa Naendelea vizuri, alhamdulillah, japo nina maumivu makali sana. NINAWASHUKURUNI NYOTE KWA JITIHADA ZENU, SALA, MAOMBI NA UPENDO MKUBWA MLIONIONESHA. ALLAH ATAWALIPA KILA LENYE KHEIR! Amin. #AllahAkbar''


Waziri huyo alipata ajali ya gari Agosti 4 mwaka huu eneo la Magugu, Manyara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad