Mwamauziki wa Uganda aliyegueka kuwa mwanasiasa Bobi Wine amepigwa na vikosi vya usalama na hawezi kuzungumza wala kutembea , mawakili wake wanasema.
Mbunge huyo wa upinzani amefikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi katika mji wa kaskazini Gulu, alikoshtakiwa kwa mashtaka mawili ya kumiliki silaha kinyume cha sheria na shtaka moja la kupatikana na silaha , lakini sio uhaini kama ilivyoripotiwa awali.
Alikamatwa baada ya gari lililokuwa kwenye msafara wa rais Museveni kushambuliwa Jumatatu katika mji wa Arua, kufuatia kuwadia uhaguzi mdogo ulioshindaniwa vikali.
Dreva wa Wine baadaye alipigwa risasi na kuuawa, katika kinachotajwa na mbunge huyo kuwa ni jaribio la kumuua yeye.
Bobi Wine supporters pose with his posterHaki miliki ya pichaAFP
Image caption
Wakosoaji wanasema Bobi Wine amelenga kushinikiza umati tu lakini hajawasilishwa miswada bungeni kwa masuala anayoyapigania katika kampeni
Mshirika wake Kassiano Wadri, aliyeshinda uchaguzi huo wa Arua, awali alishatkiwa na uhaini akiwa pamoja na wengine 31.
Serikali haijatoa tamko kuhusu tuhuma kwamba Bobi alishambuliwa akiwa kizuizini.
Mbunge huyo mwenye miaka 36 kwa muda mrefu amekuwa akiikosoa wazi serikali ya Uganda.
"Wakati viongozi wetu wamekuwa wapotoshaji na watesaji. Wakati uhuru wa kujieleza unalengwa na kukandamizwa, nafasi yetu inakuwa ni ya upinzani."
Hayo ni maneno katika wimbo unaoitwa Situka, iliyo na maana sawa na Zinduka, aliouimba Wine kufuatia kuwadia kwa uchaguzi mkuu mnamo 2016.
Alitumia wimbo huo kuwashinikiza Waganda wawajibike kupambana na rushwa na ukandamizaji nchini mwao.
Kwa wakati huo wasanii wengi nchini wa zamani walimuunga mkono raisi Yoweri Museveni kuchaguliwa tena lakini Wine alikataa kuingia kwenye mkondo huo.
Bobi Wine aliwashinda wagombea kutoka kwa chama kikuu cha siasa katika uchaguzi mdogo mwaka jana na kuibuka kuwa mbunge
Ni hapo watu walishuku kwamba huenda Wine alitaka kuingia katika siasa.
Nyota huyo wa mtindo wa Afrobeats aliingia katika taaluma ya muziki katika miaka ya 2000, hna anaelezea kipaji chake kuwa ni cha kuelimisha na kuburudisha. Mojawapo ya vibao vyake vya awali Kadingo, inahusu usafi wa mwili.
Jina lake rasmi Wine, ni Robert Kyagulanyi Ssentamu, alichaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mdogo baada ya kusimama kama mgombea huru mwaka jana wilayani Kyadondo mashariki, Uganda ya kati.
Aliwashinda wagombea kutoka chama tawala National Resistance Movement (NRM) na chama kikuu cha upinzani Democratic Change (FDC).
Baada ya kutangazwa mshindi, aliahidi kuangazia zaidi kuwaunganisha raia.
"Jambo langu la kwanza ninalotaka kufanya ni kufanikisha maridhiano kati ya viongozi wa Kyadondo Mashariki...Ninataka siasa zitulete pamoja... jinsi muziki ufanyavyo."
Mawakili wa Bob Wine: Bobi Wine Hawezi Kuzungumza Wala Kutembea
0
August 17, 2018
Tags