Mbasha Matutu Awajibu TFF Baada ya Kula Kifungo katika Soka

Mbasha Matutu Awajibu TFF Baada ya Kula Kifungo katika Soka
Aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji (TFF) na Msimamizi wa Kituo cha Michezo Shinyanga, Mbasha Matutu, ameibuka na kulijibu Shirikisho la Soka Tanzania baada ya kumfungia maisha kutojihusisha na masuala ya soka.

Kamati ya Maadili iliyokutana Jumamosi Agosti 25,2018 Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) imemfungia kutojishughulisha na Mpira wa Miguu maisha Matutu kwa makosa matatu ya kushindwa kutekeleza majukumu yake,ubadhirifu,kughushi na kuiba kinyume na kanuni za Maadili na Ligi Kuu.

Akizungumza na Radio Magic kupitia kipindi cha michezo, Matutu amesema haoni harasa yoyote juu ya kufungiwa kwake huku akieleza kulipokea jambo hilo kwa furaha kubwa.

Alipoulizwa kuhusiana na kukata rufaa, Matutu alisema hana muda huo hata kidogo kwasababu jambo hilo amelipokea kwa furaha na amani tele hivyo atakuwa anakula kuku kwa raha mustarehe.

"Ni jambo zuri, ni jambo ambalo ukilipokea unapaswa kusherehea vizuri zaidi> Sina uda wa kukata rufaa kwa maana halina mantiki ya kulifanyia maamuzi hayo" alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad