Mbosso Akabidhiwa Hati ya Mjengo wa Maana na WCB Asema Anawahamishia Wazazi Wake

Mbosso Akabidhiwa Hati ya Mjengo wa Maana na WCB Asema Anawahamishia Wazazi Wake
Msanii wa muziki kutoka label ya WCB, Mbosso amefunguka kuzungumzia nyumba ambazo walijengewa na Mkubwa Fella wakati yupo Yamoto Band. Nyumba hizo ni nne za wasanii wote ambao walikuwa Yamoto Band zipo Mbande Kisewe, Chamazi jijini Dar es salaam.


Akiongea katika kipindi cha The Playlist ya Times FM, Mbosso amesema nyumba yake kwa sasa ipo tayari na ameshakabidhiwa kila kitu kwaajili ya kuanza kuitumia kama nyumba yake.

“Nyumba ipo na Mkubwa ameshanikabidhi kila kitu na mwezi wa tisa nitawapeleka wazazi wangu wakakae huko mimi nibaki hapa mjini,” alisema Mbosso.


Muimbaji huyo mwenye nyimbo 6 toka ajiunge WCB, amesema kwa sasa maisha yake yamebadilika kwa kiasi kikubwa tofauti na awali.

Wiki iliyopita Mbosso pamoja na Lavalava walikabidhiwa magari na bosi wao Diamond Platnumz.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad