Mbowe: Waliomuua Akwilina Wanajulikana, Lakini Wanataka Sisi Ndo Tufungwe


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amesema Tanzania inapitia kipindi kigumu cha viongozi wa kiserikali kutoheshimu sheria na katiba.

Akizungumza na wandishi Leo Makao Makuu ya Chama hicho, Mbowe amesema kumekuepo na uvunjifu wa sheria kwenye kesi inayomkabili yeye na viongozi wengine wandamizi wa Chama hicho huku wakiwa wananyimwa haki zao za msingi.

" Tunaheshimu mahakama zetu lakini kinachofanyika Hivi Sasa sio haki kwetu, hii ni kesi ambayo inawahusisha wabunge ambao wanapaswa kuwepo katika majimbo yao lakini kesi imekua ikipelekwa pelekwa tu muda mwingine hadi usiku.

" Mawakili wetu walipeleka maombi ya kutaka kesi yetu ipelekwe mahakama kuu kutoka kisutu lakini hakimu amekataa na kulazimisha tuingie kwenye shtaka jambo ambalo Wakili Mtobesya amekataa kukubaliana nalo na kuamua kujitoa mbaya zaidi Hakimu ametaka kesi iendelee kesho," Amesema Mbowe.

Mbowe amesema ubabe unaotumika na dola katika kuwakandamiza wapinzani katika kesi yao, uonevu wanaofanyiwa katika chaguzi zinazoendelea, utishwaji wa viongozi wao kutoka kwa viongozi ambao wanasaidiwa na Polisi utapelekea kutokea kile kinachoendelea nchini Uganda.

" Tunaheshimu mahakama lakini inawezekana mahakimu na majaji kutumika kwa kufanya kazi kwa maelekezo, na hii lazima tuzungumze ili Dunia na watanzania waelewe kwamba hatuoni haki ikitendeka kwa kesi yetu inayosikilizwa na hakimu Mashauri na ndio maana hata tulipoomba ajitoe ameendelea kukataa.

“Waliomuua Akwilina wapo, lakini tunatengenezewa kesi sisi ili tufungwe, tunasema hatuogopi kwenda jela, lakini tunataka tufungwe pale ambapo tuna haki ya kufungwa. Waue wengine, wapige risasi wengine, waumize wengine, walioonewa ndiyo wanakuwa washutumiwa?” amesema Mbowe
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Chanzo... Ni utashi wenu kutengeneza mkusanyiko...

    Sababu ..ni nyinyi kuto tii wito Na kujioneaha ubabe WA kuwa TUNAWEZA

    Visingekuwepo hivyo viwili hapo juu..AKWILONA WETU ANGEKUWEPO HAI...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad