Mbunge Avitaja Vijiji vyenye Majina ya Sehemu za Siri za Wanaume na Wanawake

Kila mtu alilazimika kuuficha uso wake katika bunge la Ghana siku ya Alhamisi baada ya mbunge mmoja kuorodhesha baadhi ya majina ya vijiji katika eneo bunge lake ambayo yanashirikisha majina ya sehemu za siri za wanaume na wanawake.

Mbunge Frimpoing Osei alikuwa akimuuliza waziri wa kawi kuhusu usambazaji wa umeme katika maeneo kadhaa ya eneo bunge lake la Abirem.


Katika kanda ya video anaonekana akitaja majina ya Etwe nim Nyansa, Kote Ye Aboa na Shua ye Morbor - na tatizo lilikuwa kutafsiri majina hayo kwa lugha ya kiingereza.


  • Etwe nim 
  • Nyansa Kote Ye Aboa 
  • Shua ye Morbor

Majina hayo yamewaacha raia wengi wa Ghana ambao walikuwa hawajayasikia kabla ya kutajwa katika bunge kushindwa yalitoka wapi.

Mwandishi wa BBC Thomas Naadi nchini Ghana anasema kuwa majina hayo hutolewa na maselta wa kwanza kwa jamii na yanatokana na maisha ya watu wa jamii hizo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad