Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea Apingana na Takukuru

Mbunge wa Temeke Abdallah Mtolea Apingana na Takukuru
Mbunge wa Temeke (CUF), Abdallah Mtolea ameipinga taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Temeke ambayo ilieleza kuwa kiasi cha Shilingi milioni moja kiliokolewa baada ya kuidhinishwa kutolewa katika mfuko wa jimbo bila ya kuwepo kwa uthibitisho wake.

Mtolea ameieleza East Africa BreakFast ya East Africa Radio, leo Jumatano Agosti 8, 2018 kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa mfuko wa Jimbo la Temeke na kwamba chini yake hakuna jambo la aina hiyo ambalo limewahi kutokea, kwani fedha za mfuko hazitoki bila kuidhinishwa kwenye kikao cha kamati.

“Jimbo la Temeke ni langu, hakuna kitu kama hicho na hiyo ripoti walimhoji nani wakati mimi kama mwenyekiti wa mfuko wa jimbo sina taarifa? Mbona sijawahi kupata hata dokezo na hiyo hela iliyozuiwa iko wapi?”, amesema Mtolea.

Agosti 3, 2018 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke ilipokea jumla ya taarifa 458 yakiwemo malalamiko na vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi kwa kipindi cha miez 12 ambapo jumla ya majalada ya uchunguzi 274, huku zaidi ya shilingi milioni 62 zimeokolewa na kurejeshwa serikalini kufuatia udhibiti wa mianya ya rushwa ikiwemo milioni moja ya mfuko wa maendeleo ya jimbo kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad