Club ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta leo imeshuka tena uwanjani kucheza game ya 4 ya Ligi Kuu Ubelgiji dhidi Charleroi katika uwanja wao wa nyumbani Luminus.
Mbwana Samatta leo ameichezea KRC Genk game ya Ligi Kuu Ubelgiji dhidi ya Charlero kwa dakika 34, hiyo ni baada ya kuingia dakika ya 54 akitokea benchi na kwenda kuchukua nafasi ya Zinho Gano aliyecheza kwa dakika 54 za kwanza.
KRC Genk leo imevuna point tatu lakini hadi Mbwana Samatta anaingi game ilikuwa 1-1, Genk ikitoka kusawazisha goli dakika ya 45 kupitia kwa Jere Uronen, hiyo ni baada ya Charleroi kupata goli la kuongoza mapema dakika ya 27 kupitia kwa Cristian Benavente.
Mbwana Samatta alianza kuonesha makali yake dakika ya 77 baada ya kuifungia Genk goli la pili na baadae dakika ya tatu za nyongeza akafunga goli la tatu la Genk kwa mkwaju wa penati, hiyo inakuwa ni game ya tatu mfululizo kwa Mbwana Samatta kuichezea Genk na kufunga, Genk wapo nafasi ya pili kwa kuwa na point 10 nyuma ya Anderletch wanaoongoza Ligi kwa kuwa na point 12.