Mchezaji Simon Msuva Akaribishwa TP Mazembe


Lubumbashi, DR Congo. Mabingwa mara tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, TP Mazembe kesho Jumanne itashuka kwenye uwanja wake la nyumbani la Stade du 5 Juillet 1962, mjini Lubumbashi kuikaribisha Difaa El Jadidi ya Morocco, anayoichezea mshambuliaji mahiri wa Tanzania, Simon Msuva.

Mazembe inacheza mchezo huo ikitoka kuvuna pointi moja ya ugenini ilipotoka 1-1 na ES Setif ya Algeria, Agosti 17 mwaka huu, bao lao likifungwa na Kabaso Chongo.

Matokeo hayo yaliipa uongozi wa kundi B ikiwa na pointi 11, na uhakika wa kuongoza kundi wakati wa upangaji ratiba za robo fainali.

Kwa upande mwingine Difaa, nayo itaingia uwanjani ikikumbukia ushindi wa mabao 2-0 wa nyumbani ilipoialika MC Alger, mabao yake yakifungwa na Bilal El Megri na Simon Msuva.

El Jadida inacheza mechi zake zote za mwisho ugenini baada ya mchezo huu itacheza michezo miwili dhidi ya ESS na MCA za Algeria.

Mchezo huo dhidi ya Difaa kwenye Uwanja wa TP Mazembe wa du 5 Juillet 1962 utachezeshwa na mwamuzi kutoka Seychelles, Bernard Camille.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad