Mfanyakazi Aiba Ndege ya Abiria na Kuiangusha Seattle Marekani

Mfanyakazi aiba ndege ya abiria na kuiangusha Seattle Marekani
Mfanyakazi mmoja wa shirika la ndege ameiba ndege isiyo na abiria kutoka uwanja wa ndege wa Seattle na kuiangusha karibu na kisiwa kilicho karibu.

Mamlaka zinasema kuwa mwanamume huyo alipaa na ndege hiyo bila ruhusa siku ya Ijumaa usiku saa za Marekani na kusababisha uwanja wa ndege kufungwa.

Rubani 'mlevi' atolewa katika ndege ya Uingereza
Ndege mbili za jeshi za F15 ziliifuata ndege hito. Haijulikani ikiwa mwanamume huyo alinusurika baada ya ndege hiyo kuanguka.

Polisi mkuu kaunti ya Pierce alisema kuwa hicho sio kitendo cha kigaidi akiongeza kuwa mwanamume huyo ni wa eneo hilo mwenye miaka 29

Ndege isiyo na madirisha yazinduliwa
Waelekezi wa ndege walijaribu kumshawishi mwanamume huyo kutua kabla ndege hiyo kuanguka.

Ndege hiyo ilikuwa aiana ya Horizon Air Q400, kwa mujibu wa taarifa ya shirika, mshirika wa Horizon la Alaska Airlines. Ilianguka kusini mwa kisiwa cha Ketron karibu na kituo cha kijeshi.

Kwenye kanda moja ya video mwanamume huyo anaweza kusikika akiwa na wasi wasi kuhusu ni kiasi gani cha mafuta alikuwa nacho. Pia alisema kuwa angetua mwenyewe kwa sababu alikuwa anafahamu kupitia michezo ya kompiuta.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad